Home Habari za michezo IKIWA IMEPITA MIEZI KADHAA TOKA ASEPE ….HITIMANA KAONA ISIWE TABU…KAFUNGUKA HAYA KWA...

IKIWA IMEPITA MIEZI KADHAA TOKA ASEPE ….HITIMANA KAONA ISIWE TABU…KAFUNGUKA HAYA KWA SIMBA…


MAKOCHA wawili wakubwa ndani ya Afrika, Mcongo, Raoul Shungu wa AS Vita na Mnyarwanda, Thiery Hitimana wa KMC aliyewahi kukaimu nafasi ya Kocha Mkuu Simba, wamekubali muziki na kusema Wekundu wa Msimbazi wanaweza kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Shungu amesema mpaka sasa anaona Simba inaonyesha ubora mkubwa katika mechi zake za Caf. Hadi sasa Simba ni kinara wa Kundi D ikiwa na pointi 7, ikifuatiwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast yenye pointi 6, Berkane ya Morocco (pointi 6) na USGN (pointi 4).

Simba itavaana na ASEC leo Jumapili katika mchezo mgumu ugenini lakini Wekundu wana uhakika wa kutinga robo fainali kama wakishinda mechi moja tu kati ya mbili zilizobakia. Watamaliza hatua ya makundi kwa mechi ya nyumbani Dar dhidi ya USGN ya Niger.

“Simba hawakuwa na timu mbaya lakini sikutegemea kama wengeweza kuwa na ubora ambao wapo nao kwa sasa lakini ukiangalia wanavyocheza kwenye mechi zao, ni wazi unaona ni watu ambao wana kitu wanakitafuta licha ya kuwa na sura mpya katika baadhi ya nafasi lakini bado wanaonyesha siyo timu ya kubezwa kabisa.

“Naamini watafika fainali na uwezo wa kufanya hivyo wanao kulingana na mechi ambazo zimebakia katika kundi lao, ushindani na ubora wao umekuwa mkubwa kiasi cha kuweza kupata matokeo mazuri wakiwa katika uwanja wowote tofauti na misimu miwili nyuma katika mechi za kimataifa walitegemea kushinda wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani,” alisema Shungu.

Kwa upande wake Hitimana, amesema Simba siyo tu kwamba inaweza kufika fainali, bali inaweza pia kubeba ubingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha huyo ambaye aliachana na Simba mwanzoni mwa msimu huu, amesema: “Simba wanaweza kuchukua ubingwa kutokana na nafasi waliyopo sasa. “Kwa asilimia na alama walizonazo sasa, naweza kusema asilimia 80 wana uwezo wa kuchukua ubingwa kutokana na uwezo wao wa ndani na wa nje ya uwanja.”

SOMA NA HII  WAKATI ONYANGO AKIZIDI 'KUWADINDIA....MABOSI SIMBA WAPANIA KUPINDUA MEZA KIBABE ...