Home news KUHUSU WANAOM’BEZA KUWA HATAIWEZA NAFASI YA CHAMA…BWALYA AWAJIBU HIVI

KUHUSU WANAOM’BEZA KUWA HATAIWEZA NAFASI YA CHAMA…BWALYA AWAJIBU HIVI


KIUNGO wa Simba Larry Bwalya, amefunguka mipango yake msimu huu kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabigwa, huku akisema watafanya vizuri.

Mzambia huyu huu ni msimu wake wa pili akiwa na Simba na sasa anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji watakaowika zaidi msimu huu.

Mzambia huyo amesema kuwa anaamini atakuwa na msimu bora sana.

“Nimejipanga vizuri kuisaidia timu yangu kwenye Ligi ya Mabingwa na hata Ligi Kuu Bara naamini kuwa kazi hiyo naiweza

“Ligi ni ngumu ila tushaizoea tutapambana kutetea nafasi yetu kwa kuwa uwezo huo tunao,” alisema Bwalya.

SOMA NA HII  FT: SIMBA SC 0-1 ARTA SOLAR....GOLI LAO LAFUNGWA NA MTANZANIA...'STRAIKA MZUNGU' AZIDI KUPEPESUKA...