Home Uncategorized BREAKING:NIYONZIMA ASAINI YANGA

BREAKING:NIYONZIMA ASAINI YANGA


KLABU ya Yanga leo Desemba 18 imeongeza mkataba na kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima kutokana na Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze kukubali uwezo wake.


Nyota huyo raia wa Rwanda amekuwa kwenye uwezo mkubwa ndani ya kikosi hicho licha ya kukosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Kiungo huyo ambaye anaushkaji pia na nyavu akiwa ametupia bao moja kati ya 22 ambalo alifunga mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa ameongeza dili la mwaka mmoja. 

Niyonzoma alirejea kikosini baada ya kusepa na kuibukia nchini Rwanda ambapo alikwenda kujiunga na timu ya taifa ambayo ilikuwa inashiriki michuano ya Afcon.

Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa Kaze ametoa ripoti ambayo itatumika kwenye usajili.

Ripoti hiyo imeelekeza wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo na wale ambao wataongezwa ndani ya kikosi hicho ambacho kesho kitakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

“Tupo vizuri kwa ajili ya kufanya usajili ambao ni pendekezo la mwalimu, ripoti ipo tayari na tutaitumia katika kuboresha kikosi ili kiwe bora.

“Wapo wachezaji ambao wataongeza mkataba ndani ya timu, wengine wataondolewa kwa mkopo pia wapo ambao wataongezwa ndani ya timu.

“Tayari tumekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza ambaye yeye kila kitu kimekamilika kilichobaki kwa sasa ni mwalimu mwenyewe kuamua kumtumia akiona inafaa,” . 
SOMA NA HII  YANGA MZIGONI NOVEMBA 15, AZAM COMPLEX