Home news WAKATI ‘FEI TOTO’ AKITAKIWA MOROCCO…MZUVA AIBUKA NA HILI…ADAI KUTAKA KUJUA UKWELI WOTE..

WAKATI ‘FEI TOTO’ AKITAKIWA MOROCCO…MZUVA AIBUKA NA HILI…ADAI KUTAKA KUJUA UKWELI WOTE..


NYOTA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayecheza kwa sasa Wydad Casablanca amemjaza upepo kiungo fundi wa Yanga, Feisala Salum ‘Feitoto’ anayetajwa kuhitajiwa na klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco.

Msuva aliyewahi kuichezea El Jadid kabla ya kutua Morocco, amesema ni muda sahihi kwa fundi huyo wa Kizanzibar kufanya maamuzi ya kutoka nje ili kufuata nyayo zake na pia kupanua upeo wake kisoka kama ilivyo kwake.

Difaa El Jadida inatajwa kuwa miongoni mwa klabu tatu ambazo zipo kwenye vita ya kuwania saini ya Feisal ambaye kwa sasa ni moto wa kuotea mbali, ikiwemo Horoya AC ya Guinea aliyotoka Heritier Makambo.

Msuva anaamini, Yanga hawawezi kumzuia Feisal endapo wakipokea ofa nzuri kama ilivyokuwa kwake 2017 baada ya kuisaidia timu hiyo ya Wananchi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara yao ya mwisho.

“Nimepanga kuongea na uongozi wa Difaa kujua ukweli wa hizo taarifa, binafsi nimezifurahia kwa sababu Feisal ni mchezaji mzuri na anaweza kufanya vizuri hata huku nje na ikawa faida kwa timu yetu ya taifa,” alisema Msuva na kuongeza;

“Wachezaji wa Kitanzania wanatakiwa kuchangamkia nafasi ambazo zinapatikana za kwenda nje na sio lazima wazisubiri muda mwingine wanatakiwa kuwa tayari kuzipambania, tunatakiwa tutoke kama ambavyo wageni wamekuwa wakiingia kwenye ligi yetu na kuongeza chachu ya ushindani.”

Msuva aliyewahi kuzichezea Moro United na Yanga iliyomuuza El Jadid alisema amekuwa akiongea na Fei na kumweleza uwezekano wakutoboa anga na kufanya vizuri nje ya Tanzania, “Unajua tunaweza kuwa tunashauriana lakini maamuzi ya mwisho yapo mikononi mwake.”

Wiki tatu ziliopita Msuva alikuwa nchini kwa mapumziko mafupi na alipata nafasi ya kwenda kambini kwa Yanga na kubadilishana mawazo na benchi la ufundi la timu hiyo, wachezaji pamoja na viongozi mbalimbali.

Takwimu za Feisal, zinamuonyesha mchezaji amehusika kwenye mabao mengi msimu huu 2021/2022.

Kwenye michezo tisa aliyocheza amepachika mabao manne na kutoa asisti nne, ikiwa na maana kahusika na mabao nane kati ya 14 iliyonayo Yanga.

SOMA NA HII  RAIS SAMIA ATIA NENO KIPIGO CHA SIMBA JANA....WENYEWE WAKIRI KUZIDIWA...