Home Habari za michezo RAIS SAMIA ATIA NENO KIPIGO CHA SIMBA JANA….WENYEWE WAKIRI KUZIDIWA…

RAIS SAMIA ATIA NENO KIPIGO CHA SIMBA JANA….WENYEWE WAKIRI KUZIDIWA…

Habari za Simba

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Simba ijipange kwaajili ya msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutolewa kwenye robo fainali ya michuano hiyo na bingwa mtetezi Al Ahly jana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Misri

Rais Samia ameandika kwenye mitandao yake ya kijamii “Mchezo mzuri Simba. Usiku haukuwa wa ushindi lakini tumeziona juhudi na zinatupa faraja na matarajio kuwa, msimu ujao wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika mambo yatakuwa mazuri zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha.”

Simba imeishia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara ya nne katika misimu sita baada ya kupokea kichapo cha jumla ya mabao 3-0 na Al Ahly bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Simba imepoteza ugenini mabao 2-0 Cairo yakifungwa Amr El Solia dakika ya 47 na Mahmoud Kahraba kwa penalti dakika ya 90 huku bao la kwanza lilifungwa na Ahmed Nabil Koka Machi 29, katika Uwanja wa Mkapa.

Katika hatua nyingine, Klabu ya Simba imeeleza kuwa haikuwa bahati kwao kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya wachezaji wa timu hiyo kumwaga jasho jingi kwa ajili ya nembo ya timu yao .

Simba imeondoshwa na Al Ahly kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya jana usiku kukubali kichapo cha mbao 2-0 huko nchini Misri katika mchezo wa robo fainali mkondo wa pili.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa timu hiyo wamechapisha ujumbe wenye kutia moyo wachezaji pamoja na mashabiki wa Simba huku wakipania michuano mingine iliyosalia.

“Mashujaa wetu walipambania nembo ya Simba na Tanzania lakini bahati haikuwa kwetu. Kimataifa tumemaliza lakini mashindano ya ndani yanaendelea, nguvu zetu tunahamishia huko ili kufanya vizuri.”

SOMA NA HII  MASHABIKI CONGO WATUMA VIDEO KWA ENG HESRI NA YANGA KUTAKA MSAADA...ISHU IKO HIVI...

2 COMMENTS

  1. Simba Sports Club tatizo lipo kwa viongozi na hawa ndio wa kulaumiwa kwa kununua wachezaji wasiokua na hadhi ya wachezaji wanaotakiwa kuwepo na ahadi ambazo hazitimii mojawapo ya Manzoki hawakutimiza ahadi kwa timu , mashabiki , na wanachama pamoja na wapenzi
    Mangungu
    Try Again na Kajula hawa wanatakiwa waondoke kwenye Uongozi

  2. Simba inahitaji kuongeza nguvu kwenye ulinzi na umaliziaji vinginevyo utakuwa mchezo wa piga nikupige tu na mwisho wake ni kipigo hatarii