Home Uncategorized MOLINGA APOTEZWA JUMLAJUMLA KWA MABAO NA KIUNGO HUYU WA SIMBA

MOLINGA APOTEZWA JUMLAJUMLA KWA MABAO NA KIUNGO HUYU WA SIMBA


HASSAN Dilunga, Kiungo mshambuliaji ambaye ni mzawa amempoteza mshambuliaji namba moja wa Yanga, David Molinga raia wa Congo kwenye mechi nne za mwezi Januari ambazo ni sawa na dakika 360.
Simba iliyo chini ya Sven Vanderbroeck, ndani ya mwezi Januari imecheza jumla ya mechi nne imefunga mabao 11 na kinara wa kutupia ni Dilunga mwenye mabao matatu huku Yanga iliyo chini ya Luc Eymael imecheza jumla ya mechi nne na imefunga mabao matano na kinara wa mabao ndani ya Yanga ambaye ni Molinga amefunga bao moja.
Dilunga ameanza kuonyesha makeke yake chini ya Sven ambapo ametupia jumla ya mabao matano na pasi moja ya bao huku Molinga akiwa chini ya Eymael amefunga bao moja ndani ya mwezi Januari mbele ya Singida United.
Eymael alisema kuwa kinachomponza Molinga ashindwe kufunga mabao mengi ni kutotulia ndani ya uwanja jambo analolifanyia kazi ana imani atafunga mabao mengi msimu huu.
SOMA NA HII  MASTAA WATANO WA SIMBA NJE KIKOSI CHA KWANZA LIGI IKIREJEA