Home Uncategorized MABOSI JUVENTUS WAMSHUSHIA LAWAMA CR 7 KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA ULAYA

MABOSI JUVENTUS WAMSHUSHIA LAWAMA CR 7 KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA ULAYA

UONGOZI wa Juventus umemshushia lawama nyota wao namba moja ,Cristiano Ronaldo kuwa anatumia njia nyingine mbadala ya kutaka kuondoka ndani ya timu hiyo baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Raia huyo wa Ureno anaishia kwenye hatua ya 16 bora tangu mwaka 2010, alikuwa kwenye kikosi kilichotolewa hatua ya 16 bora usiku wa kuamkia leo wakati timu yake ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Lyon ila walitolewa kwa faida ya bao la ugenini kwa kuwa mchezo wa kwanza Lyon ilishinda bao 1-0 kabla ya janga la Corona.

Mabingwa hao wa Seie A wametolewa jumla kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo watashuhudia bingwa akipatikana wakiwa nyumbani.

Kiongozi wa Juventus, Andrea Agnelli amesema kuwa inawezekana kuwa ni mwanzo wa nyota huyo kushinikiza kuondoka ndani ya Juventus huku ikitajwa kuwa anahitaji kwenda PSG ili kuungana na Neymar Jr na Kylian Mbappe. 

Kiongozi huyo amesema kuwa ana imani na nyota huyo anaweza kubaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa ni mchezaji muhimu ila kwa sasa ni nguvu ya vyombo vya habari inamvuruga.

Mabao yalifungwa na Cristiano dakika ya 43 kwa penalti na dakika ya 60 huku lile la Lyon likifungwa na Memphis Depay dakika ya 12 kwa penalti.

SOMA NA HII  MKUU WA MKOA WA DAR, MAKONDA APEWA CHEO NDANI YA SIMBA