Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…MBRAZILI SIMBA AANZA KUWASHA MITAMBO…ATAKA WIKI TANO YA KUFA MTU..

KUELEKEA MSIMU UJAO…MBRAZILI SIMBA AANZA KUWASHA MITAMBO…ATAKA WIKI TANO YA KUFA MTU..

Habari za Simba leo

Kama kuna kitu mashabiki wa Simba wanasubiri basi ni kujua nyota wao wapya wa msimu ujao, lakini kocha Robert Oliveira ‘Robertinho amebainisha kuwa watu washasajiliwa na wiki tano zinatosha kwake.

Robertinho akiwa nchini Brazil amefurahia ripoti ya mabosi wake ya kuwasainisha nyota wapya, akisema hadi sasa mwendo ni mzuri katika kumletea watu ambao watairudisha heshima ya Wekundu wa Msimbazi.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, kocha huyo alisema mabosi wake watakapomaliza usajili huo atahitaji wiki tano pekee kuingia nao kambini Ulaya kuandaa kikosi cha ubingwa msimu ujao.

Simba imepanga kuweka kambi nchini Uturuki kujiandaa na msimu mpya wakiachana na kambi za Afrika kwa muda baada ya kuweka kambi Misri msimu uliopita.

“Kawaida tunahitaji wiki nane kujiandaa na msimu mpya, lakini kutokana na ishu ya muda, mimi hata nikipata wiki tano tu zinatosha kumaliza kazi ya kutengeneza timu,” alisema Robertinho ambaye hajapoteza mechi yoyote ya ligi msimu uliopita.

“Nafurahia kazi ya viongozi wangu huko Tanzania, ripoti wanayonipa inanipa raha mpaka sasa tuko salama kuwapata mastaa wote ambao tumewataka kwa ajili ya kuijenga timu mpya.

“Tumeshampata mshambuliaji ambaye pia anaweza kucheza kama winga niliyekuwa namuhitaji, nadhani kwa rekodi zake zinazozijua sasa ni wakati wake kuja kuyaleta makali hayo hapa Simba.”

Aidha katika ratiba hiyo ya maandalizi, Robertinho alisema Simba itahitaji mechi zisizopungua nne za kirafiki, ambazo zitakuja kupima kwa nyakati tofauti ubora wao kabla ya kurudi nchini.

“Tutaanza na mechi nyepesi zaidi na baadaye tunaweza kucheza na timu za daraja la katikati na ile wiki ya mwisho tunaweza kuanza kucheza na timu ngumu, nitafurahi kama tutakapokwenda litakuwa eneo la kutupa mechi za namna hiyo,” alisema.

SOMA NA HII  WAKATI ONYANGO AKIZIDI 'KUWADINDIA....MABOSI SIMBA WAPANIA KUPINDUA MEZA KIBABE ...