Home Habari za michezo FEI TOTO GUMZO MKUTANO MKUU YANGA…ISHU YAKE YAMALIZWA HIVI…

FEI TOTO GUMZO MKUTANO MKUU YANGA…ISHU YAKE YAMALIZWA HIVI…

Fei toto Azam FC leo

KLABU ya Yanga imetangazo mapata ya mauzo ya wachezaji waliyowapata msimu uliyopita huku mchezaji aliyeuzwa ni kiungo Feisal Salum.

Yanga ilimuuza Feitoto kwa Azam FC kwa dau lililofichwa kwa pande hizo mbili, lakini waliwekeana vipengele ambavyo timu hizo zitaendelea kunufaishana kwa mchezaji huyo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick amesema bajeti ya mapato na matumizi iliyotumika msimu uliopita huku akitaja mapato waliyoyapata kwa upande wa mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kwa mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwenda Azam ambapo awali dili lake halikuwekwa wazi.

“Mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kama mnavyojua tumeweza kumuuza Feisal Salum ‘feitoto” amesema Sabri

Feisal amesaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya akae kwenye timu hiyo ya Chamazi hadi 2026.

SOMA NA HII  MWAMBUSI: TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here