Home Habari za michezo HII HAPA CV YA KOCHA MPYA YANGA…MFUMO ANAOTUMIA KUNA TIMU ITAKULA NYINGI...

HII HAPA CV YA KOCHA MPYA YANGA…MFUMO ANAOTUMIA KUNA TIMU ITAKULA NYINGI AISEE..

Kocha Mpya Yanga Miguel Angel

BAADA ya kuondoka kwa Nasreddine Nabi, Yanga imemtangaza Miguel Angel Gamondi kuchukua mikoba yake.

Kocha huyu mwenye uraia wa Argentina na Italia ana umri wa miaka 56 na anapenda kutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Kwa mara ya kwanza kuongoza timu kama kocha mkuu ilikuwa mwaka 1998 ambapo alikuwa kocha wa Racing Club ya Argentina ambayo alidumu nayo hadi mwaka 1999.

Baada ya kuachana na timu hii mwaka uliofuatia 2000, alitua rasmi barani Afrika ambapo alifanya kazi chini ya kocha Oscar Fullone kuinoa Al-Ahly ya Libya kisha akaungana nae kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Burkina Faso.

Baada ya hapo akala shavu la kuifundisha Esperance kama kocha msaidizi lakini akadumu kwa miezi isiyozidi saba kuanzia Januari 7, 2004 hadi Juni 30, 2004.

Julai 01, 2005 alitua Mamelod Sundown ambapo kwa mara ya kwanza alijiwekea rekodi ya kufundisha timu ya Afrika kama kocha mkuu kwenye maisha yake ya ukocha.

Alidumu Mamelodi kwa mwaka mmoja na miezi miwili na akafungashiwa virago Oktoba 03, 2006 ikiwa ni miezi kadhaa tu tangu ulipoanza msimu mpya wa 2005/06.

Kocha Mpya Yanga Miguel AngelBaada ya Mamelodi alitua Hassania ya Morocco ambayo aliifundisha kuanzia Januari 2007 hadi Novemba mwaka huo huo.

Alirudi tena nchini Afrika ya Kusini kuifundisha Platinum Stars ambayo ndio timu pekee aliyokaa muda mrefu akihudumu kuanzia mwaka Desemba 13, 2007 hadi Mei, 2009 akiiongoza kwenye mechi 50, akishinda 17 sare 16 na kufungwa 17.

Julai 04, 2010 alitua kwa wababe wa Algeria CR Belouizdad ambayo aliiongoza kwenye mechi 30, ikishinda 13 sare tisa na kufungwa nane, akaondoka Juni 2011.

Julai mwaka huo huo akatua zake Al-Ittihad Kalba SC ya huko Dubai ambayo aliifundisha hadi Juni, 2012.

Mwezi mmoja baadae yaani Julai, 2012, akarudi tena Afrika kuifundisha USM Alger ambayo alidumu hapo kwa miezi mitatu na siku 17 kabla hajafungashiwa virago Oktoba 17, akioongoza timu hiyo kwenye mechi sita ikishinda mbili sare moja na kufungwa tatu.

Baada ya kufutiwa kibarua na USM, alirudi tena CR Belouizdad, bapo alihudumu kwa nusu msimu kuanzia Juni 20, 2013 hadi Januari 01, 2014 lakini matokeo mabaya kwenye mechi 15 ambapo CR Belouizdad ilishinda nne, sare tatu na kufungwa nane ndio yalisababisha afungashiwe virago kabla hata msimu haujamalizika.

Aliamua kuachana kidogo na masuala ya kufundisha na badala yake alijiunga na Hassania d’Agadir ya Morocco kama Mkurugenzi wa ufundi kuanzia mwaka 2015 hadi 2017.

Kutokana na timu kufanya vibaya mabosi wa timu hiyo wakamtaka Miguel arudie tena kufundisha na akapewa rasmi mikoba ya kuinoa timu hii kuanzia Julai 01, 2017 hadi Novemba 20, 2019 alipoiongoza kwenye mechi 75.

Akapata tena shavu lakuwa Mkurugenzi wa ufundi wa Wydad Casablanca kwa miezi 10 kuanzia Januari 2020 hadi Novemba mwaka huo huo.

Baada ya kuondoka Wydad aliajiriwa na MAS Fes inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco na hapa akadumu kwa miezi miwili na siku kadhaa na akafurushwa kutokana na kiwango kibovu cha timu ambapo katika mechi saba alizokuwa anaiongoza ilishinda moja tu, sare tano na kufungwa moja.

Timu yake ya mwisho kuifundisha ilikuwa ni Ittihad Tanger ya Morocco ambayo inapatikana kwenye Jiji la Tanger lililopo karibu na mpaka kati ya Morocco na Hispania.

Hapo alifanya kazi kuanzia Novemba 30, 2021 hadi April 26, 2012 akiiongoza kwenye mechi 11, ikishinda nne, sare moja na kufungwa sita, tangu hapo hakuwahi kuifundisha timu yoyote na leo ndio ametangazwa kuwa kocha mpya wa Yanga.

Katika safari yake yote hiyo mafanikoo makubwa aliyowahi kuyapata kama kocha ni kuchukua kombe la FA LA Morocco akiwa na Hassania mwaka 2019, vilevile akiwa Mkurugenzi wa masuala ya ufundi wa Wydad aliiwezesha timu hii kumaliza nafasi yapili kwenye Ligi Kuu nchini Morocco.

SOMA NA HII  YANGA YAKIMBIZA KWA MAPATO YA MLANGONI 2020/21