Home Habari za michezo HIVI NDIVYO SENZO ALIVYOKIMBIA NA ‘SIMBA YAKE’ KUELEKEA YANGA…..

HIVI NDIVYO SENZO ALIVYOKIMBIA NA ‘SIMBA YAKE’ KUELEKEA YANGA…..

Habari za Simba

Nimekiangalia tena Kikosi cha Yanga cha Mwaka 2018, nimekiangalia kikosi cha Simba cha mwaka huo pia, kisha nimeviangalia vikosi vyao mwaka huu 2023 miaka mitano baadaye. Project ya Yanga inaonesha muendelezo lakini project ya Simba kuna sehemu ilikatika na ndipo hapo inaleta shida.

Simba ilikua na wakati mzuri wa Soka na ilifuata weledi wa Kazi na kisha kumleta Senzo Mbatha (Malume) kama CEO wao kisha kwa namna yao na Ukubwa wa SENZO Wakafikiri wanaiweza Afrika lakini Ukweli ni Kwamba PROJECT ya Senzo ndio inawatesa Simba. Baada ya Senzo Simba imekua klabu isiyokua na muendelezo wa Project zake na sasa wanajitafuta.

Senzo ndiye mwanadamu anayelifahamu zaidi soka la Afrika kuwahi kuhudumu Simba na baadaye Yanga. Baada ya Senzo akaja Barbara Gonzalez ambaye kimsingi alikuja kuifikisha Simba wodi ya wagonjwa, Barbara hakua mtu anayelifahamu soka la Afrika kwa level ya Senzo hivyo kwa nafasi ya kuendeleza Project ya Senzo ilikua ni kuimaliza Simba.

Tazama Tofauti, Yanga wakamchukua Senzo, wakampa kazi na baada ya mafunzo ya kiundeshaji Senzo akaondoka zake na Uongozi mpya ukaingia kisha akafuata MJANJA mwingine Andre MTINE. Ukiwatazama Yanga wanakua, wanamuendelezo tofauti na Simba, Yanga hawasumbuki hata kwenye kuiseti timu na mipango yao.

Baada ya Kuingia Barbara na Kuondoka kwake ndipo Simba iliingia Shimoni. Tusiwalaumu viongozi hawa, Project iliyumba na kwa level ya Kushindana Barani Afrika huwezi kufanya mabadiliko makubwa inabidi uungeunge ndicho kinachowakuta SIMBA. Kwa hali waliyonayo hivi sasa na wasipotoa Macho watakuja kupata aibu ya mwaka huko Mbeleni..!

Timu ya Simba imechoka, unahitaji wachezaji si Chini ya Kumi wenye Umri wa Ubora na ubora wa kukupa matokeo kwa level ya Ushindani Barani Afrika. Kwa miaka minne ya Robo Fainali barani Afrika Simba ilipaswa kujua wanavukaje kwenye awamu ya Tatu, Awamu ya Kwanza ugeni, pili Bahati Mbaya na awamu ya Tatu kipimo cha Ubora.

Ameandika Biko Scanda.

SOMA NA HII  MPANGO WA MANGALO KUMRITHI PASCAL WAWA MSIMBAZI UKO HIVI