Home kimataifa ENGLAND WASHINDA, UBAGUZI WA RANGI WATAWALA

ENGLAND WASHINDA, UBAGUZI WA RANGI WATAWALA


 BAADA ya kulikosa taji la Euro 2020 timu ya taifa ya England imeanza kwa mwendo matata katika mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia ikiwa ni namba moja katika kundi I baada ya kufikisha pointi tano kwa kuwa ilishinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Hungray.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Puskas Arena ilikuwa ni mabao ya Raheem Sterling alipachika bao dk 55, Harry Kane dk 63,Harry Maguire dk 69 na Declan Rice dk 87.Pia suala la ubaguzi wa rangi lilitawala katika mchezo huo kutoka kwa mashabiki wa Hungary jambo ambalo limeelezwa kuwa linafanyiwa uchunguzi.

Ushindi huo wanaupata ikiwa ni baada ya siku 53 kuyeyuka tangu timu hiyo ipoteze kwa mikwaju ya penalti mbele ya timu ya taifa katika mchezo wa fainali ya Euro 2020, Uwanja wa Wembley.

Licha ya England kushinda bado kulikuwa na hali ya ubaguzi wa rangi ambapo ripota wa Sky Sport, Rob Dorsett aliyekuwa uwanjani hapo amesema kuwa alikuwa akisikia watu wakizungumza kuhusu ngedere baada ya mguso wa mpira wa kwanza kwa Sterling pamoja na muda ambao Kane alipiga goti ishara ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England, Gareth Soutgate amesema kuwa kazi lazima ifanyike katika kupinga ubaguzi wa rangi sio kwenye mpira pekee bali katika maisha yote.

SOMA NA HII  YANGA YAJIBU MAPIGO SIMBA..NABI ACHEEKA..MASHABIKI SIMBA WAWEKA REKODI CAF...