Home Habari za michezo BAADA YA KUWASASAMBUA WAZAMBIA JANA…MBRAZILI SIMBA KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI…

BAADA YA KUWASASAMBUA WAZAMBIA JANA…MBRAZILI SIMBA KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Power Dynamos kwenye kilele cha Simba Day.

Robertinho amesema kikosi chake  kinazidi kuimarika siku hadi siku na wachezaji wanazidi kuzoeana kitu ambacho kinampa wigo mpana wa uchaguzi wa timu.

Robertinho ameongeza kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa wameonyesha uwezo mkubwa na wanazidi kuzoea mazingira ya timu pamoja na wenzao.

“Nimefurahishwa na kiwango cha timu, tumecheza vizuri na timu inazidi kuimarika. Tuna kikosi kizuri.

“Hata wachezaji wapya tuliowasajili wameonyesha uwezo mkubwa, na wanazidi kuzoea mazingira mapya pamoja na wenzao,” amesema Robertinho.

Robertinho amewashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la Simba Day na kulifanya kupendeza zaidi.

SOMA NA HII  MSAMAHA WA CHAMA WAMUIBUA MATOLA....AFUNGUKA A-Z HALI ITAKAVYOKUWA...