Home Habari za michezo BAADA YA KURUDI RASMI NA KUKIWASHA JANA…MIQUISSONE APEWA ZA USO KWA UNENE...

BAADA YA KURUDI RASMI NA KUKIWASHA JANA…MIQUISSONE APEWA ZA USO KWA UNENE WAKE…

Habari za Simba

Wakati kwa mara ya Kwanza wachezaji wa Simba wakonekana hadharani jana Agosti 6 katika kilele cha Tamasha la “Simba Day” katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia

Wapo nyota kadhaa wageni ambao wamesajiliwa dirisha hili wameonekana kuanza na moto mkubwa kama Straika Willy Onana na Kiungo Fabrice Ngoma ambao walianza kwa kutupia magoli katika mchezo wa jana.

Nyota alieteka hisia za wengi katika usajili wake ni Jose Luis Miquissone ambae nae alipata nafasi ya kucheza mchezo wa jana kwa dakika chache.

Sasa Mchambuzi wa Michezo kutoka TV3 Alex Ngereza ambae hapo awali alipingana na usajili wa mchezaji huyo amezungumza kuhusu kiwango kilichooneshwa na Miquissone jana;

“Kiwango cha Miqusson kimeshuka sana sidhani kama anaweza kurudi kwenye ubora wake kwasababu hata hivyo amekuwa mnene sana tofauti na alivyokuwa kipindi cha nyuma”

Je una neno lipi la kumwambia Mchambuzi Alex Ngereza? Unakubaliana na maoni yake?

SOMA NA HII  KENEDY JUMA:ILIKUWA NDOTO YANGU KUCHEZA MASHINDANO YA KIMATAIFA