Home Habari za michezo WAKATI AZIZI KI AKISINYA MKATABA MPYA YANGA….NABI, WYDAD WATIA DAU KUMCHOMOA PACOME…

WAKATI AZIZI KI AKISINYA MKATABA MPYA YANGA….NABI, WYDAD WATIA DAU KUMCHOMOA PACOME…

Habari za Yanga leo

Walichofanya Klabu ya Yanga ni kutocheza na shilingi chooni, wakaamua kutoa mkataba wa muda mrefu kwa Kiungo Mshambuliaji wao, Stephane Aziz Ki ambao utamuweka jangwani kwa miaka mingine mitatu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Aziz Ki ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, tayari ameshasaini mkataba na Yanga na kilichobakia ni kuweka hadharani juu ya makubaliano hayo.

Mkataba wa awali wa Aziz na Yanga unafikia ukingoni Juni 2024, na amehusishwa na vilabu vya Afrika Kusini ikiwemo Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates zote zikihitaji huduma ya kiungo huyo wa Burkina Faso.

Wakati huo huo,Taarifa zinaeleza kuwa Wydad Casablanca ya Morocco na AS FAR Rabat (inayofundishwa na Kocha Nasreddine Nabi) zinamfatilia Kwa karibu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Yanga SC, Pacome ZouZoua.

Klabu hizo zinalenga kumsajili nyota huyo kwenye dirisha kubwa usajili mwaka huu ambapo Wydad wao wapo kwenye maboresho makubwa kuelekea msimu ujao.

FAR Rabat wanataka kuongeza ubora kwenye kikosi chao ambapo wamekuwa Bora Kwa msimu takribani miwili lakini wanataka kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa msimu ujao.

SOMA NA HII  KAZE BYE BYE YANGA NAFASI YAKE YACHUKULIWA NA MCAMEROON HUYU