Home Habari za michezo LWAMBANO:- PESA ANAYOTOA MO DEWJI NDANI YA SIMBA HAITOSHI….

LWAMBANO:- PESA ANAYOTOA MO DEWJI NDANI YA SIMBA HAITOSHI….

Habari za Simba SC

Mtangazaji wa michezo wa kituo cha radio cha Clouds FM, Alex Luambano amesema kuwa tatizo lililopo Simba SC kwa sasa ni mwekezaji wao Mohammed Dewji ‘Mo’ kwani ameshindwa kutoa pesa kwa ajili ya usajili na uendeshaji wa mambo mbalimbali ya timu na badala yake timu amewaachia wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo.

Luambano amesema hiyo ndiyo sababu kubwa ya Simba SC kuyymba na kupata matokeo mabovu ikiwemo kuishia robo fainali ya CAFCL, na robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.

“Kwa uchunguzi wangu nilioufanya sasa hivi anayewasumbua Simba, wanashindwa kukaa sawa ni mwekezaji wao Mohammed Dewji.

“Mohammed Dewji sasa hivi ndio tatizo la Simba kama wanasimba hawajui, toka alipoacha nafasi yake, timu kaitelekeza. Viongozi waliopo kwenye bodi ndio wanaopambana kujichangisha na kuhakikisha timu inakwenda.

“Timu ikifanya vizuri mashabiki wanatoa credit kwa Mo,lakini Mo yupo mbali na Simba, Simba inaendeshwa kwa fedha za CAF, udhamini na kujichangisha, Mo hatoi hela.

“Msimu ukiisha hela ambayo Mo anatoa ni Bilioni 2.4 katika Bilioni 20 aliyowekeza ambayo kiuendeshaji haitoshi,” amesema Luambano.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA