Home Yanga SC BALAMA MAPINDUZI AREJEA NCHINI KUTOKEA SAUZ

BALAMA MAPINDUZI AREJEA NCHINI KUTOKEA SAUZ

 KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Balama Mapinduzi amerea nchini leo akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa ajili ya matibabu.

Akiwa Afrika Kusini, Balama alifanyiwa upasuaji wa enka na kutokana na upasuaji huo anatarajiwa kuwa nje kwa kipindi cha wiki tano.

Akizungumzia kuhusu matibabu ya mchezaji huyo Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassani Bumbuli amesema: Balama Mapinduzi amerejea leo kutokea nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji, tunatarajia atakuwa nje kwa wiki tano na baada ya hapo tutatoa taarifa zaidi,”

Naye Balama amesema: “Nawashukuru wote ambao wamenisaidia kukamilisha matibabu yangu, naomba mzidi kuniombea ili Mungu akipenda basi nirejee uwanjani,”

SOMA NA HII  BOSI YANGA ASHINDWA KUJIZUAI ISHU YA 'SURE BOY' KUSAJILIWA YANGA...AANIKA YOTEE...