Home Habari za michezo BAADA YA KUONA YANGA NA SIMBA ZILIVYOCHEZA JANA….KMC WAJIPIGAPIGA KIFUANI NAKUUTAKA UBINGWA...

BAADA YA KUONA YANGA NA SIMBA ZILIVYOCHEZA JANA….KMC WAJIPIGAPIGA KIFUANI NAKUUTAKA UBINGWA WA LIGI..

Uongozi wa KMC umeweka wazi kuwa unahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

KMC chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imekusanya pointi 13 baada ya kucheza mechi 8 za ligi, imeshinda tatu, sare nne na imepoteza mchezo mmoja ikiwa nafasi ya tatu.

Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa ubora wa pira kodi, pira mapato unaonekana na kila mpinzani anawahofia.

β€œUnaona namna ambavyo tunacheza hadi raha, wachezaji wana morali kubwa na wanatimiza majukumu yao malengo yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa ligi kwani ligi bado inaendelea.

β€œTumekuwa kipimo sahihi kwa timu zote ambazo zinacheza mechi za kimataifa na tumecheza na Azam FC, Simba nadhani mashabiki waliona namna kazi ilivyokuwa na bado tunazidi kuonyesha ubora wetu,” amesema Mwagala.

SOMA NA HII  SI GOLINI TU....HIVI NDIVYO 'MADEMU' WANAVYOMPAPATIIA MAYELE BONGO...NTIBAZONKIZA AFUATIA...