Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISA….SIMBA NA AZAM ZATEGEA TAMKO LA YANGA KUHUSU NABI…AKIFUKUZWA TU...

ZA NDAANI KABISA….SIMBA NA AZAM ZATEGEA TAMKO LA YANGA KUHUSU NABI…AKIFUKUZWA TU WANAYE…

Habari za Yanga SC

Wakati taarifa zikidai mabosi wa Yanga wanafikiria kufumua benchi lao la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi, Za Ndaani Kabisa zinasema wenzao Azam FC wanasikilizia maamuzi hayo, ili wambebe Mtunisia huyo.

Habari za ndaani Kabisa zinasema kumetokea mgawanyiko ndani ya uongozi wa Yanga wakipinga juu ya hatua ya kuondoshwa kwa kocha wao Nabi ambaye amekalia kuti kavu ikiwa ni siku chache baada ya timu yao kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo, mpango huo umekumbana na upinzani mkubwa baada ya vigogo wengine kupinga uamuzi huo.

Upande mwingine mashabiki wa Yanga wanaomnyesha kutokukubaliana na uamuzi huo wakiona Nabi bado anafaa kuendelea kuwa kocha wao baada ya kusikia taarifa hizo.

Wakati Yanga hali ikiwa hivyo wenzao Azam wanasubiria maamuzi hayo wakimvizia Nabi ili akachukue mikoba ya Mfaransa Denis Lavagne ambaye tayari wameachana naye.

Azam hawajakubaliana na Lavagne hasa baada ya timu yao kutupwa nje ya Kombe la Shirikisho kisha kupoteza tena mchezo wa tatu wa Ligi dhidi ya KMC wiki hii.

Matajiri hao wa Chamazi wanasubiri maamuzi hayo kama ilivyo Simba kuvizia huduma ya Nabi kuja kufundisha moja ya timu hizo.

Ikumbukwe pia kuwa, jana Oktoba 23, wakati wa Dabi ya Simba na Yanga, aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uganda, Milutin Sledojevic (Micho) alikuwa katika Jukwaa na Viongozi wa Yanga akishuhudia mtanange huo.

Baadhi ya taarifa ziliripoti kuwa Kocha huyo amekuja nchini kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Yanga ili kuchukua mikoba ya Nabi huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Micho anaelekea Azam FC.

Hata hivyo Uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hizo na kusema kuwa Micho ni shabiki wa Yanga na alikuja kushuhudia mchezo huo kama watu wengine waliofika kutazama dabi hiyo kubwa zaidi Afrika Mashariki.

SOMA NA HII  KISA SIMBA NA MASHINDANO YA SUPER LEAGUE...UWANJA WA MKAPA KUPIGWA MSASA UPYAA...