Home Ligi Kuu SERIKALI YATOA TAARIFA KUHUSU KUYEYUKA KWA MECHI YA SIMBA V YANGA

SERIKALI YATOA TAARIFA KUHUSU KUYEYUKA KWA MECHI YA SIMBA V YANGA

TAARIFA kuhusu mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga ambao ulipaswa kuchezwa Mei 8, 202i Uwanja wa Mkapa ila uliahirishwa kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda ule wa awali kwa kuwa ni kinyume na kanuni.


Taarifa iliyotumwa leo Mei 11 kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa ilipokea maelekezo yaliyotolewa Bungeni  jana Mei 10 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Usiku wa Mei 10, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amekutana na kufanya kikao na mashauriano na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF), Bodi ya Ligi, Baraza la Michezo Nchini, (BMT) na Klabu za Simba na Yanga.

Taarifa imeeleza kuwa kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dk. Hassan Abbasi, Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT, Bibi Neema Msita, Rais wa TFF, Wallace Karia na Katibu Wilfred Kidao.

Pia Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Bwa.Stephen Mghuto na Mtendaji wake Almas Kasongo. Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na Mjumbe wa Bodi ya Simba, Zacharia Hanspope na kwa upande wa Yanga ni Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla aliyeambatana na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Yanga, Mhandisi Bahati Mwaseba na Kaimu Katibu Mkuu, CPA Haji Mfikirwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa viingilio vitarudhishwa kwa mashabiki 43,947 kwa mashabiki waliokata tiketi zao kupitia N-Card na Waziri amesema amewaomba mashabiki kuwa watulivu katika kipindi hiki na kuiamini Serikali kuwa ilikuwa na nia njema na sababu za msingi iliposhauri awali kwa wadau wa mchezo huo kuwa mechi isogezwe mbele kwa saa chache kabla ya kujitokeza mazingira yaliyosababisha Bodi ya Ligi kulazimika kuaahirisha kabisa mchezo huo.

Kuhusu hatma ya mechi hiyo makubaliano yamefikiwa kuwa mechi hiyo irudiwe ili kuwapa wapenzi wa soka kile walichokitarajia.

Taarifa hiyo imeeleza namna hii:-
 

 

SOMA NA HII  FT: MTIBWA 0-0 SIMBA SC...PABLO AENDELEA KUTESEKA MIKOANI...CHAMA 'AKIKUNA NA KUKISHA' HASWA...