Home Ligi Kuu FT: MTIBWA 0-0 SIMBA SC…PABLO AENDELEA KUTESEKA MIKOANI…CHAMA ‘AKIKUNA NA KUKISHA’ HASWA…

FT: MTIBWA 0-0 SIMBA SC…PABLO AENDELEA KUTESEKA MIKOANI…CHAMA ‘AKIKUNA NA KUKISHA’ HASWA…

 


DAKIKA 90, zimekamilika katika uwanja wa Manungu kwa wenyeji Mtibwa Sugar kulazimishwa suluhu ya 0-0, na mabingwa watetezi Simba.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikishambuliana kwa zamu katika lango la mwenzake huku umakini ukionekana kuwa mkubwa kwa pande zote mbili katika kuokoa mashambulizi.

Kiungo mpya wa Simba, Clatous Chama alicheza mchezo wake wa kwanza msimu huu tangu asajiliwe na klabu hiyo akitokea RS Berkane ya Morocco alipoingia katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya kiungo mwenzake Hassan Dilunga.

Huo unakuwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa Simba kushindwa kuibuka na ushindi baada ya mchezo uliopita kufungwa bao 1-0 na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Januari 17, huku kwa upande wa Mtibwa Sugar ikiwa ni sare ya pili mfululizo baada ya kufungana bao 1-1, na Ruvu Shooting Januari 14.

Matokeo hayo yanawafanya Simba kuendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 25, baada ya kucheza michezo 12, nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 32, huku Kwa upande wa Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya 13 na pointi 12 baada ya kucheza michezo 13.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI BONGO...APEWA SHAVU UBELGIJI...KUKIPIGA NA SAMATTA