Home Uncategorized JOSE MOURINHO AKASIRIKA KWELI KISA SARE

JOSE MOURINHO AKASIRIKA KWELI KISA SARE


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Hotspur aligomea mkutano wa waandishi wa Habari baada ya mchezo wake dhidi ya Bournemouth kukamilika kwa sare ya bila kufungana.

Mourinho,jana Julai 9, alikasirishwa na maamuzi ya VAR pamoja na mwamuzi Paul Tierney kwa kuamini kuwa wote walikuwa na maamuzi mabaya kwani alistahili kupata penalti baada ya mchezaji wake Harry Kane kusukumwa akiwa na mpira ndani ya eneo la penalti.

Baada ya mchezo huo kukamilika Mourinho hakuwa na furaha, aliingia chumba cha mahojiano alipoulizwa kama anasikia kupitia headphones alijibu hapana kisha akazivua headphones na kuacha kuongea bila kusubiri tatizo hilo lifanyiwe kazi.

Sare hiyo inawafanya Spurs wawe nafasi ya 9 wakiwa na pointi 49 huku Bournemouth ikiwa nafasi ya 18 na pointi 28 zote zikiwa zimecheza mechi 34.

Alipoingia kwenye chumba cha habari alipoulizwa na ripota:’Jose Mourinho unaniskia? alijibu “Hapana” na kuvua headphones kisha akaondoka jumla.

SOMA NA HII  AZAM FC YATHIBITISHA KUACHANA NA CHECHE NA MAGANGA, YAWATAKIA KILA LA KHERI