Home Yanga SC NI RASMI, MWAMBUSI TENA YANGA

NI RASMI, MWAMBUSI TENA YANGA


KLABU ya soka ya Yanga imemtangaza aliyekuwa kocha wao msaidizi Juma Mwambuzi kuwa kaimu kocha wa Yanga akichukua nafasi ilioachwa na kocha Cedric Kaze.

Yanga juzi Jumapili ilifikia maamuzi ya kuvunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa na kocha Cedric Kaze, kutokana na mwenendo mbaya wa timu, ambapo kati ya michezo sita iliyopita ya Ligi Kuu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee.

Mpaka anaonyeshwa mlango wa kutokea juzi usiku, Kaze alikuwa ameiongoza Yanga kwenye jumla ya michezo 25, akishinda michezo 16, amefungwa michezo miwili na kutoa sare mechi saba.

Akizungumzia maamuzi hayo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla amesema: “Tunategemea mwalimu Mwambusi ataichukua timu wakati tunatafuta mwalimu mkuu.

“Bahati nzuri yeye aliondoka vizuri, amepata matibabu klabu imemsaidia kwenye matibabu yake amepata nafuu. Hana ugeni wa timu tulikuwa nae kwenye Mapinduzi Cup kwa hiyo kurudi kwake sio jambo geni.

“Mwalimu mwingine tutaendelea na taratibu nyingine za kawaida, makocha watatuma CV zao zitakwenda kamati ya ufundi watazipitia na kuona yupi anafaa kwenye klabu yetu kwa sasa.”

SOMA NA HII  ORODHA YA NYOTA SITA YANGA AMBAO MIKATABA YAO INAELEZWA KUFIKA UKINGONI