Home Uncategorized HAWA JAMAA NI WAZEE WA MIPENALTI, MBABE WAO HUYU HAPA

HAWA JAMAA NI WAZEE WA MIPENALTI, MBABE WAO HUYU HAPA

KWENYE Ligi Kuu Bara kazi kubwa kwa washambuliaji ni kutupia kila wapato nafasi ila kuna wataalamu wa kupiga mipira iliyokufa yaani penalti.

Hawa jamaa mbali ya kufunga kwenye harakati za kumalizia pasi za mwisho ila wamefunga pia kwa penalti namna hii:-

Peter Mapunda Mapunda anakipiga Mbeya City ametupia mabao tisa kati ya hayo sita amefunga kwa penalti.

Meddie Kagere anakipiga Simba, ametupia mabao 19 kati ya hayo tatu amefunga kwa penalti.

Sixtus Sabilo anakipiga Polisi Tanzania ametupia mabao saba kati ya hayo mawili amefunga kwa penalti.
Marcel Kaheza anakipiga ndani ya Polisi Tanzania ametupia mabao saba kati ya hayo mawili ametupia kwa penalti.

Ayoub Lyanga anakipiga Coastal Union ametupia mabao 7 kati ya hayo mawili amefunga kwa penalti.

SOMA NA HII  HAO YANGA WANABALAA WAMCHAPA MTU NANE