Home Uncategorized BEKI KISIKI NDANI YA INTER MILAN AIPIGIA HESABU MANCHESTER UNITED

BEKI KISIKI NDANI YA INTER MILAN AIPIGIA HESABU MANCHESTER UNITED


BEKI kisiki wa Inter Milan Diègo Godin ameingia kwenye anga za kuwindwa na Spurs pamoja na Manchester United.

Godin hajawa na maisha mazuri ndani ya Inter Milan kwa kukosa nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu Antonio Conte ambaye amekuwa akimsifu kuwa ni beki bora.

Ndani ya Serie A akiwa na Conte amefanikiwa kucheza mechi 16 huku beki tegemeo wa kati akiwa ni Alessandro Baston.

Tayari nyota huyo ameanza kupiga hesabu za kusepa ndani ya Serie A na chaguo lake ni Manchester United.

SOMA NA HII  IDRISA SULTAN BADO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI