Home Uncategorized KOCHA AS VITA ABARIKI MOZIZI KUTUA YANGA…AFUNGUKA MAAJABU YAKE..!!

KOCHA AS VITA ABARIKI MOZIZI KUTUA YANGA…AFUNGUKA MAAJABU YAKE..!!

PALE DR Congo kuna kocha mmoja mkongwe ambaye amewahi kufanya kazi Yanga na amesikia klabu yake hiyo inamsaka ‘top straika’ mmoja Mpiana Mozizi akawasisitiza wafanye fasta sana.

Kocha ambaye ameyazungumza hayo ni Raoul Shungu ambaye amewahi kuifundisha Yanga na kuwapa mafanikio kwa kutwaa mataji mbalimbali amesema kama hesabu za Yanga ni kweli wanamtaka Mozizi basi jamaa ni mshambuliaji bora aliyekamilika. Shungu ameliambia Mwanaspoti Mozizi ni mshambuliaji bora na wala hajabahatisha kuwa juu ya msimamo wa ufungaji akiwa na mabao 12 na hata Simba wakimpata pia atawasaidia kimataifa.

“Huyu ni mshambuliaji mzuri sana nasikia hayo maneno pia naona kwenye vyombo vya habari huko Tanzania Yanga wanamtaka Mpiana,” alisema Shungu.

“Mpiana hapa ndio anaongoza kwa kufunga mabao anafunga sawa na mchezaji wetu Fiston (Mayele) na Muleka (Jackson) wa TP Mazembe hao wote wanafunga idadi sawa.”

Akimchambua kwa ubora wake Shungu alisema Mozizi anaijua kazi yake ya kufunga na wala sio mshambuliaji mwepesi kukabika kutokana na kiu yake ya kutamani kufunga kila mchezo.

Kocha huyo msaidizi wa AS Vita inayoongozwa na Florent Ibenge alisema Mozizi anajua kufunga kwa kichwa na hata miguu lakini pia ana nguvu sana.

“Hapo Tanzania watu wanataka mchezaji kama Mpiana ana nguvu sana hakati tamaa anafunga kwa miguu na hata kichwa na beki akimsahau au akafanya makosa kidogo tu ameumia atakuwa ameshafunga.

“Yanga nawajua na mpira wao kama wana mawinga wazuri na hata viungo wengine wanaojua kumpa nafasi atawafanyia kazi kubwa sana.

Yanga wanabahati ya kupata wachezaji wazuri kutoka hapa lakini pia wana viongozi ambao hapa Congo wanaheshima kubwa kwahiyo sioni kama watapata shida kumpata Mpiana,”alisema Shungu.

“Hata wachezaji wa hapa wanapenda kuchezea timu zenye mashabiki wengi kama Yanga au Simba sasa Yanga kama watampata watafurahia na hata Mpiana mwenyewe akifanya vizuri atafurahia maisha ya hapo, Tanzania kuna mashabiki wengi wanapenda timu zao sana,” aliongeza Kocha huyo anayezungumza kiswahili kizuri.

SOMA NA HII  BILIONEA YANGA AFUNGUKA MKATABA WA YANGA NA LA LIGA