Home news BAADA YA KUHAMIA YANGA…MANARA ATOA MSHAHARA WAKE WOTE KWA MATHIAS MDAMU..AMTAJA GSM

BAADA YA KUHAMIA YANGA…MANARA ATOA MSHAHARA WAKE WOTE KWA MATHIAS MDAMU..AMTAJA GSM


Mfanyabiashara na bilionea wa Yanga, Ghalib Said Mohamed wa GSM ametoa Sh6 Milioni kama mchango wake kwa ajili ya matibabu ya Mathias Mdamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msemaji Mpya wa Yanga, Haji Manara alisema Ghalib ameguswa na tukio hilo la Gerard kupata majeraha hivyo kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha ambacho kitamsaidia katika matibabu yake.

“Ghalib ni mtu wa watu na kama wengine walivyojitokeza kumchangia mchezaji huyo wa Polisi Tanzania nae pia ameguswa na kutoa mchango wake ambapo tutaukabidhi sehemu husika, lakini hata mimi nimeguswa na najitolea kumchangia,” alisema Manara.

Manara alisema anamchangia Mdamu kiasi cha Dola 300 (zaidi ya 600,000) na Sh10,000, ikiwa ni sawa na jumla ya Sh700,000.

“Natoa laki saba ambayo ni mshahara wangu wa Julai kama sehemu ya kumchangia Mdamu ambaye sote kwa ujumla tunajua hali anayopitia,” alisema Manara.

Itakumbukwa akiwa Simba SC, Manara alinukuliwa kuwa analipwa Tsh Laki saba kwa mwezi, hivyo ametoa mshahara wake wa mwisho kulipwa na Simba kwa Mdamu

Katika hatua nyingine Manara alisema wao kama viongozi wa Yanga wataendelea kumchangia Mdamu ili kuhakikisha anapona na kurejea katika hali yake ya kawaida.

“Huu ni mwanzo tu ila malengo yetu kama Yanga kwa ujumla ni kumsaidia Mdamu kupata matibabu zaidi ili tumuone akirejea kwenye majukumu yake ya kila siku kama walivyo watu wengine,” alisema.

Wadau mbalimbali wa michezo nchini wamekuwa wakiguswa na kuamua kumchangia Mchezaji huyo huku wengi wao wakiandaa mechi za hisani ili tu kuhakikisha wanapata fedha ambayo itamsaidia katika matibabu yake.

Mathias Mdamu alivunjika miguu yote miwili Julai 9, wakati timu ya Polisi Tanzania ikitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC, Moshi walipokuwa wakijiandaa kwa mechi zao za kumalizia msimu uliopita na kulazwa Muhimbili upande wa Mifupa (MOI).

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA