Home Habari za michezo ALIYECHUKUA MIKOBA YA ROBERTINHO AZUNGUMZIA SARE YA JANA

ALIYECHUKUA MIKOBA YA ROBERTINHO AZUNGUMZIA SARE YA JANA

Habari za Simba leo

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Daniel Cadena amesema sare ya bao moja waliopata dhidi ya Namungo FC hakufurahia ingawa amependa jinsi walivyocheza.

Amesema ameanza kufanyia kazi mapungufu yao ikiwemo safu ya ulinzi kuruhusu bao kila mechi na ushambuliaji kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi wanazotengeneza.

Simba imeendelea kupoteza alama mbili baada ya juzi kulazimisha sare ya bao 1-1 na Namungo FC katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Kocha Cadena amesema waliweza kumiliki mchezo na kufanya mashambulizi mengi na kutengeneza nafasi ingawa hawajapata walichokitarajia.

Amesema kuwa jambo chanya ni kuwa wachezaji wameshika haraka mafunzo aliyowapa kitu ambacho anaamini katika mechi za mbele watafanya vizuri.

“Sijafurahia matokeo ya sare lakini nimependa jinsi tulivyocheza , kwa muda mfupi wachezaji wameweza kuyashika mafunzo tulioyowapa hilo jambo chanya kwangu.

Ilikuwa lazima kipindi cha pili kufanya mabadiliko kwa kutoa viungo na kuongeza washambuliaji kwa sababu Namungo walikuwa nyuma muda mrefu na wanaacha nafasi ili kuzitumia nafasi hizo,” amesema Cadena.

Ameongeza kuwa mabadiliko ya Mosses Phiri na Shaban Chilunda yalisaidia na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha na anamatarajio kutumia wiki mbili kukisuka kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ijayo ya kimataifa.

Amesisitiza kuwa anaendelea kubadilisha vitu vidogo na kuisuka timu hiyo kuwa imara zaidi na kutafuta matokeo mazuri katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo mechi ya Kimataifa ya ligi ya Mabingwa dhidi ya Asec Mimosas, Novemba 25, mwaka huu, Benjamin Mkapa Dar es Salaam

SOMA NA HII  UONGOZI WA YANGA KUNUNUA KILA GOLI LAKI 5