Home Yanga SC MSHAMBULIAJI YACOUBA APITISHWA NA MAKOCHA WA MATAIFA MANNE

MSHAMBULIAJI YACOUBA APITISHWA NA MAKOCHA WA MATAIFA MANNE


 LICHA ya kuwa na mwendo wa kobe kwenye kucheka na nyavu, mshambuliaji namba moja wa Yanga, Yacouba Songne mwenye mabao sita na pasi nne kati ya mabao 41 amepitishwa na makocha wa mataifa manne kwenye kikosi cha kwanza.

Yanga iliyo nafasi ya pili imeongozwa na makocha wanne mpaka sasa kwa msimu wa 2020/21 kutoka mataifa manne tofauti, ambapo walianza msimu na taifa la Serbia kisha Burundi,Tanzania na sasa ni Tunisia.

Amecheza jumla ya mechi 22 za ligi  kati ya 27 ambazo Yanga imecheza amekosekana kwenye mechi tano na kumfanya atumie jumla dakika 1,375.

Zama za Zlatko Krmpotic, kutoka Serbia alicheza mechi tano na kutumia jumla ya dakika 253, ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, dk 45, Mbeya City,dk 45, Kagera Sugar, dk 55, Mtibwa Sugar,dk 18, Coastal Union, dk 90.

Zama za Cedric Kaze raia wa Burundi, alitumia dakika 794 katika mechi 13 alizocheza ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, dk 63, KMC,dk 2, Biashara United,dk 8, Gwambina FC, dk 82, Simba, dk 12, Azam FC, dk 90, JKT Tanzania, dk 54, Ruvu Shooting,dk 90. Mwadui,dk 66, Dodoma Jiji dk 89, Azam FC,dk 90, Coastal Union,dk 58, Ihefu,dk 90,

Mbele ya Juma Mwambusi ambaye ni Mtanzania alicheza mechi tatu na kutumia dakika 238 ilikuwa mbele ya KMC, dk 87, Biashara United,dk 83, na mbele ya Gwambina, dk 68.

Mechi ya kwanza ya Nassredine Nabi raia wa Tunisia ndani ya Yanga alianza kikosi cha kwanza mbele ya Azam FC na aliyeyusha dakika zote 90.

Kwa sasa yupo na kikosi cha Yanga ambacho kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora, kesho Aprili 30, Uwanja wa Nelson Mandela.

SOMA NA HII  WIKI KADHAA TOKA AANZE KUKIWASHA NA YANGA....HIVI NDIVYO NABI ALIVYOICHAMBUA KAZI YA MORRISON KITAALAMU....