Home Simba SC SIMBA YAKWEA PIPA KUIBUKIA MOROCCO

SIMBA YAKWEA PIPA KUIBUKIA MOROCCO

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo kimekwea pipa kuelekea nchini Morocco. 

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho wanajipanga kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Miongoni mwa wachezaji waliokwea pipa ni pamoja na Bernard Morrison,  Meddie Kagere , Mohamed Hussein, Erasto Nyoni.

Pia kiungo wao mkabaji, Jonas Mkude ambaye alikuwa amesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na masuala ya nidhamu.

Pia Perfect Chikwenda naye yupo katika kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Peter Banda ambaye ni ingizo jipya yupo kwenye kikosi ambacho kinatarajiwa kurejea Tanzania Septemba 15.

SOMA NA HII  UKWELI MTUPU....'UTANZANIA' NA TUNACHOMFANYIA KIBU DENIS NI 'USHAMBA' MKUBWA...