Home Uncategorized SAID NDEMLA AFIKIRIA KUKIPIGA SOKA LA KULIPWA NJE

SAID NDEMLA AFIKIRIA KUKIPIGA SOKA LA KULIPWA NJE


SAID Ndemla, nyota wa Simba amesema kuwa hana hofu na uwezo wake ndani ya kikosi hicho anaamini kwamba ataweza kufikia malengo aliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.


Ndemla ni miongoni mwa wazawa ambaye jina lake lilitajwa kwenye orodha ya nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi, Oktoba 11. 


Mchezo huo ulikamilika kwa Stars kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 jambo ambalo liliwaumiza mashabiki wengi wa Tanzania ambao walijitokeza kuipa sapoti timu yao.


Ndemla amesema:”Nina amini katika kipaji na juhudi ambazo ninazo kwa sasa, imani yangu ni kwamba bado nina uwezo wa kufanya vizuri zaidi ya sasa kwa wakati ujao.


“Kikubwa ambacho kinanipa imani ni kwamba wakati uliopo mafanikio bado ninayafikiria na wakati ukifika nitayafikia kwa kuwa sijakata tamaa.


“Bado ninafikiria kuwa siku moja nitacheza nje ya Bongo soka la kulipwa hiyo ni mipango ya baadaye ila kwa sasa acha nipambane ndani ya Simba ambapo bado nipo.”

SOMA NA HII  YANGA YAZIMA HUJUMA NA JEURI ZA SIMBA