Home Habari za michezo KISA SARE YA JUZI…GAMONDI AFUNGUKA MCHEZO MBAYA WALIOANYIWA NA AL AHLY…

KISA SARE YA JUZI…GAMONDI AFUNGUKA MCHEZO MBAYA WALIOANYIWA NA AL AHLY…

Habari za Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema hajaridhishwa na matokeo ya mechi yao dhidi ya Al Ahly, hivyo sasa ameamua kuufungia kazi mchezo wa ujao dhidi ya Medeama ya Ghana ukiwa mechi ya tatu ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga juzi usiku walilazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly ya Misri, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, matokeo hayo imejitengenezea mazingira magumu ya kwenda hatua ya robo fainali za michuano hiyo.

Gamondi amesema mechi ilikuwa ya vipindi viwili, dakika 45 ya kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kutengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia lakini kipindi cha pili wapinzani wao Al Ahly waliingia kwa mipango mwingine.

Amesema Al Ahly walifanikiwa kuingiza watu wenye spidi, kipindi cha pili ambao waliwavuruga, na kukiri kuwa hawakucheza vizuri licha ya kupata bao la kusawazisha, lakini pamoja na hayo wanapaswa kusahau matokeo hayo na kuangalia mechi iliyopo mbele yao.

“Mechi ilikuwa ya ushindani mkubwa, Al Ahly wamefanikiwa katika mipango yao, sasa tunarejea uwanja wa mazoezi kusahihisha makosa yetu kuelekea mchezo ujao dhidi ya Medeama FC.

Ni mchezo huo ni muhimu kwetu kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufikia malengo yetu ya kucheza robo, tunatakiwa kupambana kushinda ugenini,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa katika uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu yao na kupigania alama tatu za ugenini dhidi ya Medeama FC, kushinda mchezo huo watajiweka kwenye nafasi nzuri ya kusaka tiketi ya kwenda robo fainali .

Katika kundi D, Al Ahly anaogoza akiwa na alama 4 , Medeama akiwa nafasi ya piliakiwa na pointi tatu sawa na CR Belouizdad wote wameshinda mechi mmoja na kupoteza moja na Yanga anashika mkia kwenye kundi hilo akiwa na pointi mmoja.

SOMA NA HII  HII HAPA SABABU YA KWANINI UACHANE NA SIMU ZINGINE UNUNUE Infinix NOTE 30 PRO AU NOTE 30 VIP..