Home Uncategorized SALAMBA: NINAPATA USHIRIKIANO MZURI KWA WENZANGU

SALAMBA: NINAPATA USHIRIKIANO MZURI KWA WENZANGU


ADAM Salamba, mtanzania anayekipiga kwa sasa ndani ya timu ya Al-Jahra SC, iliyopo Uarabuni amesema kuwa ushirikiano anaopewa na wachezaji wenzake ni mkubwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Salamba amesema kuwa amekuwa akifurahia maisha ya huko kutokana na ushirikiano anaopewa na wachezaji wenzake.

“Huku ninaishi vizuri na wenzangu, tunashirkiana vema na kila mchezaji jambo ambalo linanifanya niwe na furaha.

“Nafanya yote kutokana na kupenda kazi yangu, nipo huku ila napeperusha vema bendera ya Tanzania kwani wengi wanapenda kutambua habari za nyumbani,” amesema Salamba.

SOMA NA HII  NAMUNGO KUKUTANA NA MUZIKI WA NYOTA HAWA WA KAZI SIMBA