Home Simba SC WAWILI WAJIENGUA SIMBA, NKAMIA NA MAGUNGU WAPETA

WAWILI WAJIENGUA SIMBA, NKAMIA NA MAGUNGU WAPETA


 MWENYEKITI wa Kamati ya uchaguzi ndani ya Klabu ya Simba, Boniface Lihamwike amesema kuwa mchakato wa uchaguzi ndani ya klabu hiyo kwa sasa unaendelea vizuri huku wagombea wawili wakipita na wengine kujiweka kando.

Lihamwike amesema kuwa wagombea wawili wamebaki kutoka kwenye majina manne ambayo yalipitishwa na kamati hiyo huku majina mawili yakijiondoa.

“Wiki hii tukiwa na wagombea wanne, kamati ilipokea barua kutoka kwa wagombea wawili ambao ni Rashid Shangazi Mbunge pamoja na Hamis Tika wakiomba kujiengua kutoka kwenye mchakato huu.

“Hawa walileta barua wakiomba kujiengua kwamba walikuwa hawataki kuwa sehemu ya uchaguzi, baada ya kuleta barua kamati iliheshimu maombi yao na iliwapa taarifa za kujiondoa kwao kwenye nafasi zao.

“Hivyo Tika na Rashid hawa wana sababu zao ambazo ziliwafanya waweze kuondoka hivyo waliojiondoa wana nafasi ya kuwaambia wanachama kupitia vyombo vya habari kueleza kwa kina kwa wanajamii kwamba kwa nini waliamua kufikia hatua hiyo.

“Hivyo basi kwa heshima kubwa baada ya kamati kuwapa picha ya yale yaliyojiri mpaka leo inamtangaza Juma Nkamia mbunge mstaafu pamoja na Murtaza Magungu ambaye naye ni mbunge mstaafu.

“Hawa ni wagombea rasmi ambao wamepitishwa kugombea na kuziba pengo lililoachwa wazi na Sued Mkwabi ambaye alijiuzulu nafasi yake.

“Baada ya kuwatamka wagombea hawa kuwa ni wagombea rasmi ni rai yangu kwa Wanasimba kwa ridhaa yao kufanya maamuzi sahihi kwenye uchaguzi ili kumpata mmoja kati yao kuwa Mwenyekiti.

“Wito wangu kwa wagombea ni kwamba nawaasa wakafanye kampeni kwa ustaarabu wakizingatia kanuni na utaratibu wa Simba, kamati itafuatilia kwa ukaribu ikiwa mmoja wapo atakiuka kufanya utaratibu basi sheria itafuata mkondo.

“Kesho kamati itakaa na wagombea ili kuzungumza nao na kuwapa utaratibu wa kufanya pamoja na vitendea kazi, tunaamini uchaguzi utakuwa huru na wa haki” amesema.

 Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Februari 7,2021.

SOMA NA HII  WAKATI SAKHO AKIFANYA MAAJABU HUKO...MUGALU AMTAZAMA WEE..KISHA ASEMA YEYE NI MAYELE TU...