Home epl WEST HAM UNITED YATAKA KUSAJILI MAZIMA LINGARD

WEST HAM UNITED YATAKA KUSAJILI MAZIMA LINGARD

 


IKIWA Ole Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United atafanya maamuzi juu ya nyota wake Jesse Lingard ambaye anakipiga ndani ya West Ham United basi atapiga mkwanja mrefu.

Lingard yupo zake ndani ya West Ham United kwa mkopo na amekuwa akikiwasha kila anapopata nafasi na ameitwa timu ya Taifa ya England. 

Mpaka anaondoka West Ham United, Januari alikuwa hajacheza hata mchezo ndani ya Ligi Kuu England ila kwa sasa West Ham United wanataka kumsajili jumlajumla.

 Solskjaer amegoma kutaja kiasi cha fedha ambazo anahitaji kwa ajili ya mchezaji wake huyo zaidi ya kusema kwamba anahitaji huduma ya mchezaji wake.



SOMA NA HII  MABASI KUTOKA AFRIKA KUTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA QATAR...FAINAL ZIKISHA YATAGAWIWA BUREEE...