Home Habari za michezo MABASI KUTOKA AFRIKA KUTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA QATAR…FAINAL ZIKISHA...

MABASI KUTOKA AFRIKA KUTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA QATAR…FAINAL ZIKISHA YATAGAWIWA BUREEE…


Waandaaji wa fainali za Kombe la Dunia wameachia mabasi 1,300 kwa ajili ya majaribio ya usafiri wa umma katika kile walichokiita operesheni kubwa ya usafiri ambayo haijawahi kutokea kwa ajili ya tukio la kimataifa.

Huku zaidi ya watu milioni moja wakitarajiwa kuingia nchi hiyo ya ghuba kushuhudia fainali hizo, serikali haijasinzia katika maandalizi yake yaliyogharimu mamilioni ya dola.

Na kusafirisha mashabiki wa soka katika jiji na kati ya viwanja nane kunaonekana ndio kutakuwa changamoto kubwa kuliko yote.

“Hii ni operesheni ngumu sana ambayo haijawahi kutokea kwa ajili ya kujiandaa kwa michezo mikubwa ya kimataifa,” alisema Ahmad al Obaidly, ofisa muendeshaji mkuu wa operesheni wa Mowasalat, ambayo inaendesha huduma za mabasi na teksi nchini Qatar.

Katika jaribio la kwanza la maandalizi yaliyochukua miaka kadhaa, waandaaji walitumia ratiba ya mfano ya siku ambazo zitakuwa na shughuli nyingi katika fainali hizo, wakati mashabiki wapatao 300,000 wanaweza kuwa jijini Doha kwa wakati mmoja.

Huku kukiwa na joto kubwa, mamia ya mabasi yaliyo na viyoyozi lakini mengi yakiwa matupu yalikwenda viwanjani, kwenye stesheni za treni na sehemu za kuchukulia abiria.

Katika stesheni ya treni ya Al Wakra katika vitongoji vya jijini Doha, zaidi ya madereva 1,000 wa kampuni ya Mowasalat waliigiza kama mashabiki waliotakiwa wapelekwe Uwanja wa Al Janoub ulio umbakli wa kilomita tano.

Uwanja wa Al Bayt stadium, ambako mechi ya ufunguzi itafanyika Novemba 20, hauna stesheni yake ya treni.

Mamia ya mabasi yasiyo na abiria yalifanya safari za umbali wa kilomita 25 kwenda stesheni ya treni ya karibu katika jiji jipya la Lusail, kama itakavyokuwa kwa mashabiki wakati England itakapocheza na Marekani.

Mabasi hayo pia yalifanya safari za kurudi usiku kuendana na hali itakavyokuwa wakati wa mechi hiyo ya Kundi B itakayofanyika usiku mwingi.

“Tunataka kuhakikisha mipango yetu inakwenda sawasawa,” alisema Thani Al Zarraa, mkurugenzi wa uendeshaji wa waandaaji wa fainali hizo nchini Qatar.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIWA 'SIRIAZI' NA UBINGWA WAO...BUMBULI 'KAKUNJA MDOMO'..KISHA AKASEMA HAYA..

Obaidly alisema mabasi 3,000 yamenunuliwa na kutakuwa na zaidi ya mabasi 4,000 mitaani wakati wa fainali hizo.

Kampuni hiyo pia imedurufisha idadi ya madereva ilioajiri hadi kufikia 14,000 kwa ajili ya fainali hizo. Mengi yamenunuliwa kutoka Asia Kusini na Afrika.

Baada ya fainali hizo, mabasi ya muda mrefu yatagawiwa, ikiwa ni sehemu ya kjumbukumbu ya Kombe la Dunia, na Qatar “itakuwa moja ya nchi za kwanza kutoa huduma za mabasi ya umeme kwa usafiri wa umma,” alisemas Obaidly.