Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKIWA ‘SIRIAZI’ NA UBINGWA WAO…BUMBULI ‘KAKUNJA MDOMO’..KISHA AKASEMA HAYA..

WAKATI SIMBA WAKIWA ‘SIRIAZI’ NA UBINGWA WAO…BUMBULI ‘KAKUNJA MDOMO’..KISHA AKASEMA HAYA..


Wakati Mabingwa wa tetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Simba SC wakiwa wamedhamiria kuutetea ubingwa wao msimu huu, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amejinasibu kuwa kila mchezaji wa kikosi hicho ana uwezo mkubwa wa kufunga jambo ambalo anaamini litawapa Ubingwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania msimu huu wa mwaka 2021-22.

Bumbuli amesema hayo wakati akiongelea maandalizi ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Mlandizi ya Visiwani Zanzibar unaotaraji kuchezwa Jumatano 30 Machi 2022 huku akisema lengo la mchezo huo ni kuwapa nafasi wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kurudisha viwango vyao.

”Timu ilingia kambini tangu jumanne na tunaendelea na mazoezi kwa mujibu wa programu ya mwalimu alihitaji mechi kirafiki kwaajili ya kuwapa muendelezo wa wachezaji wetu kuwa imara kwa wale wachezaji ambao hawatumiki mara kwa mara ” amesema Hassan Bumbuli

Kwa upande mwingine Bumbuli amesema nyota wa Yanga ambao walliokuwa majeraha wamepoona na kilichosalia ninuamuzi wa Kocha Mohammed Nabi kuwatumia katika michezo ijayo ya Ligi kuu na FA.

”Hali za nyota wa Yanga Khalid Aucho, Saido Ntibanzokiza, Jesus Moloko, Crispin Ngushi zinaendelea vyema na siku yoyote wataweza kutumika katika kikosi cha Yanga ”amesema Hassani Bumbuli

Yanga ambao ni vinara wa Ligi kuu wakiwa na alama 45, utofauti wa alama 11 na wapinzani wao Simba SC wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 34 huku Yanga SC ikitarajiw kuwa Ugenini April 6, 2022 kucheza dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Chamazi nje kidg ya Jijini La Dar es salaam.

SOMA NA HII  KUHUSU SAKATA LAO NA FEI TOTO....YANGA WAPEWA NJIA HII NYEPESI YA KUMALIZA KESI KWA USHINDI...