Home Ligi Kuu PIRA KODI LEO KUCHEZWA MBELE YA POLISI TANZANIA

PIRA KODI LEO KUCHEZWA MBELE YA POLISI TANZANIA

 


CHRISTINA Mwagala,  Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania. 


Mchezo huo wa ligi utachezwa leo Machi, 4, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Christina amesema kuwa pira kodi na spana litachezwa leo.


KMC imetoka kupenya hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho baada ya kushinda mabao 5-2 dhidi ya Kurugenzi FC, Uwanja wa Uhuru jambo ambalo linawaongezea nguvu ya kufanya vizuri. 


Baada ya kumalizana na Polisi Tanzania leo, Machi 7 kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ya Tanga ambayo leo ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanba.


Christina amesema:”Tupo tayari na tunaamini kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki watupe sapoti, tunaendelea kutoa pira kodi,pira mapato na pira spana ndani ya uwanja,”.

SOMA NA HII  PANGA KUBWA LAPITA POLISI TANZANIA, 13 WAPIGWA CHINI