Home Uncategorized SAMATTA: SIKUTARAJIA KUPEWA TUZO MBILI, KAZI INAANZA LEO NIFUATE

SAMATTA: SIKUTARAJIA KUPEWA TUZO MBILI, KAZI INAANZA LEO NIFUATE

 Mbwana Samatta nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania,’Taifa Stars’ amesema kuwa hakutarajia kupewa tuzo za heshima na uongozi wa Global Group jambo ambalo limemshangaza alipotembelea ofisi za Global Group jana.

Samatta ambaye anayekipiga KRC Genk, leo atakuwa uwanja wa Taifa kumenyana na timu Kiba, kwenye mchezo wa hisani wenye lengo la kurudhisha thamani kwa jamii inayowazunguka hasa yenye mahitaji.

Akizungumza na Saleh Jembe baada ya kupewa tuzo mbili kutokana na mafanikio makubwa aliyopata katika msimu uliopita baada ya kuipa ubingwa timu yake pamoja na kufunga mabao 23 akiwa nyuma ya mfungaji bora amesema kuwa :- “Sikutarajia kupewa tuzo hizi, ni jambo kubwa na linalonipa hasira ya kupambana nasema asante kwa sapoti yenu na zawadi ambazo mmenipa ni jambo la faraja kwangu,”.

“Nitafanya kwa vitendo siku zote na kwa kuanza mashabiki wangu wasikose kujitokeza uwanja wa Taifa kuona namna nitakavyoifanya timu Kiba, kwenye Nifuate Project,” amesema.

Mhariri Mtendaji wa Global Group, Saleh Ally alitaja sababu za kutoa tuzo hizo na kusema “Tuzo hii tumempa kwa sababu amekuwa mfungaji bora karibu kila sehemu aliyokwenda pamoja na ugumu wote aliokutatana nao, ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga katika klabu zote alizopita.

“Lakini hii nyingine inasema mfano wa kuigwa Mbwana Samatta 2019, mnajua tangu amekwenda DR Congo amechukua makombe mengi, amecheza kombe la dunia ngazi ya klabu nafikiri yeye na Thomas Ulimwengu kwa Tanzania, amekuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi ya ndani na mfano wa kuigwa kutokana na kuhamasisha watu kujituma,” amesema.


SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YATUMA UJUMBE HUU KWA KMC WANA KINO BOYS