Home Uncategorized EYMAEL – KWA MORRISON TUMEHUJUMIWA

EYMAEL – KWA MORRISON TUMEHUJUMIWA

Gazeti la MWANASPOTI jana lilikueleza mapema kuwa Bernard Morrison na Jonas Mkude wameshikwa pabaya na kweli  yamewakuta. Lakini saa chache tu tangu Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuwafungia mastaa hao kucheza mechi mbili na kulipa faini ya Sh.500,000 kwa makosa ya nidhamu, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amedai kilichofanyika ni hujuma.

Kamati hiyo ya TFF ilitangaza adhabu kwa wachezaji wao wa Simba na Yanga kutocheza mechi mbili na kulipa faini hiyo, ikiwa ni zaidi ya miezi minne tangu wafanye makosa yao na kumfanya Eymael kudai kilichofanyika ni kama hujuma kwa timu yake iliyekuwa kwenye mipango yake jana.

Yanga jana ilikuwa ikivaana na Namungo, lakini mchana ikapata taarifa hizo za kufungiwa kwa winga wake huyo kwa kosa la kumpiga kiwiko, Jeremiah Juma wa Prisons kwenye mchezo wao uliopigwa Februari mwaka huu na Eymael amedai amesikitishwa na uamuzi wao ya ghafla.

Naye Mkude ameadhibiwa kwa kosa la kumpiga pia kiwiko Ally Kombe wa Biashara United mechi iliyopigwa Februri 22, lakini adhabu yake imekuwa wakati akijiuguza majeraha aliyoyapata hivi karibuni kwenye mechi yao ya kirafiki dhidi ya KMC.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti baada ya taarifa ya Morrison kuadhibiwa ambayo ilionekana kumchanganya Eymael, alisema amesikitishwa na hukumu hiyo kuchukua muda mrefu wakati ingeweza kuamuliwa mapema kwa vile TFF ina Kamati ya Saa 72.

“Hii imetusikitisha, kwani kuna makosa yalitokea tangu Januari kwenye derby yetu na Simba, lakini hakuna hukumu, leo tunajiandaa na mechi ngumu tunaelezwa Morrison kafungiwa kwa tukio la Februari, hii sio sawa,” alisema Eymael na kuongeza;

SOMA NA HII  HUWEZI KUAMINI, ILA UKWELI WOTE HUU HAPA DADIKA 630 BILA USHINDI SIMBA SC