Home Uncategorized YANGA KUIPELEKA BODI YA LIGI FIFA

YANGA KUIPELEKA BODI YA LIGI FIFA

Habari za Yanga leo

Uongozi wa Yanga umesema hawakubaliani na adhabu walizopewa na Bodi ya Ligi kwa wachezaji wao pamoja na klabu hiyo kwa ujumla tayari wameandika barua kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), CAF, FIFA, Takukuru na mamlaka nyingine kulalamika juu ya suala hilo.

Kamati ya Saa 72, Shirikisho la Soka Tanzania hivi karibuni ilitoa adhabu mbalimbali pamoja na
faini kwa klabu ya Yanga pamoja na wachezaji kutokana na makosa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Steven Mguto alitangaza kuwafungia mechi tatu na faini ya
Sh 500,000 kwa wachezaji wa Yanga, Ramadhani Kabwili, Mrisho Ngassa, Cleofas Sospeter baada
ya kugoma kutoka uwanjani katika pambano la ligi dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine Mbeya.

Yanga pia ilipigwa faini nyingine ya Sh 500,000 baada ya kushindwa kuwakilisha kikosi chake
katika mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prison, lakini katika mchezo dhidi ya Simba Yanga
walipigwa faini nyingine ya Sh 200,000 kwa wachezaji na benchi la ufundi kushindwa kutumia
vyumba rasmi vya kubadilishia nguo na faini nyingine ilikuwa ya Sh 500,000 baada ya mashabiki
wake kuwarushia chupa waamuzi.

Akizungumza na makao makuu ya Yanga, Afisa habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema
Kamati ya saa 72 imeamua kuwafungia wachezaji wao pamoja na kuipiga faini timu kwa makosa
waliotaja mbalimbali.

“Yanga hatukubaliani na adhabu hizo kwani kuna mambo mengi ya kisheria hayakufuatwa mpaka
kuamua kutoa hukumu hiyo.

“Tulipeleka malalamiko yetu mengi kwa wasimamizi wa ligi ili hatukupewa majibu, kwa maana
hiyo tumeandika barua kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), CAF, FIFA, Takukuru na mamlaka
nyingine husika kulalamika juu ya hilo,” alisema Bumbuli.
SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI WA SIMBA AOMBA NAMBA JUMLA YANGA