Home Uncategorized KAGERE AMALIZA SHUGHULI TAIFA, AACHA KILIO KWA NAMUNGO KWA BAO LAKE LA...

KAGERE AMALIZA SHUGHULI TAIFA, AACHA KILIO KWA NAMUNGO KWA BAO LAKE LA USIKU

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba leo amewanyanyua mashabiki wa timu yake kwa kufunga bao la ushindi lililoipa timu yake pointi tatu mbele ya Namungo FC.

Simba leo ilikuwa ikicheza Uwanja wa Taifa na ilianza kujipatia bao dakika ya 21 kupitia kwa Francis Kahata aliyefunga bao hilo dakika ya 21 lililosawazishwa na Bigirimana Blaise dakika ya 35 na Hassan Dilunga akafunga bao la pili akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Balora na kuwafanya Simba kuenda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili Namungo walipata bao la pili kupitia kwa Lusajo ambaye aliachia shuti kali akiwa nje ya 18 alichoambulia Kakolanya ilikuwa kuokota mpira nyavuni.

Dakika ya 88, Kagere alimaliza shughuli uwanjani kwa kufunga bao la ushindi ambalo limewapa Simba pointi tatu jumla.

Sasa inafikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya kwanza na imefunga jumla ya mabao 38.

SOMA NA HII  KUMBE NAMUNGO INABEBWA NA HIKI HAPA BONGO