Home Habari za michezo MASAU BWIRE AKUMBUSHIA ISHU YA MPAPASO…ATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA KUHUSU CAF…

MASAU BWIRE AKUMBUSHIA ISHU YA MPAPASO…ATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA KUHUSU CAF…


Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting umesema umedhamiria kucheza kwa malengo ya kupata ushindi pindi michezo yake mitatu ya mwanzo ya Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania itakapoanza ili kukwepa kushuka daraja.

Afisa Habari wa Maafande hao, Masau Bwire amesema staili ya papasa itawashughilikia timu zilizo mbele yao, dhidi ya Polisi Tanzania, Namungo, Yanga na Simba huku akichombeza kuwa Ruvu Shooting ni kubwa kwani inafiatiliwa na mashabiki wengi wa ndani na nje ya nchi.

“Walianza vibaya katika msimu huu lakini katika mechi mbili tulizocheza tumeona kikosi chetu kimebadilika na hii ni ishara tosha ya kushinda kila mchezo ambao utakuwa mbele yetu” amesema Masau Bwire.

Aidha Masau ametoa mtazamo wake katika kikosi cha Simba katika ushiriki wao wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

”Mpaka muda huu Simba bado ana nafasi ya kuvuka katika hatua ya robo fainali katika kundi hilo , kikubwa wachezaji wajitume na wapambane kupata matokeo katika uwanja wa Benjamin Mkapa wasiwa dharau Us Gender Marine” amesema Masau Bwire.

Wakati timu zingine zikipewa mapumziko lakini Maafande hao imekuwa ni tofauti wakiendelea na kambi chini ya kocha mkuu Charles Boniphace Mkwassa.

SOMA NA HII  ZA NDANI KABISA...YANGA WAMKALIA KIKAO MORRISON...MWAKALEBELA ASHIKILIA MSIMAMO..AITAJA SIMBA...