Home Habari za michezo KUELEKEA FAINAL KOMBE LA DUNIA…MASHABIKI WAZIDI KUMIMINIKA QATAR…MAUZO YA TIKETI YAVUNJA REKODI...

KUELEKEA FAINAL KOMBE LA DUNIA…MASHABIKI WAZIDI KUMIMINIKA QATAR…MAUZO YA TIKETI YAVUNJA REKODI YA DUNIA…


Jumla ya tiketi milioni 2.45 zimeshauzwa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka huu nchini Qatar baada ya zaidi ya nusu milioni kutoka katika mauzo ya raundi ya hivi karibuni, waandaaji wamesema juzi Alhamisi.

Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) limesema tiketi 520,532 ziliuzwa katika kipindi cha kuanzia Julai 5 hadi Agost 16, huku Qatar, Marekani, England, Saudi Arabia, Mexico, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ufaransa, Argentina, Brazil na Ujerumani zikiongoza kwa kununua tiketi.

Fifa imeeleza kuwa mechi maarufu katika mauzo ya tiketi ni pamoja na za hatua ya makundi baina ya Brazil na Cameroon na Serbia, Ureno na Uruguay, Costa Rica na Ujerumani, pamoja na Australia dhidi ya Denmark.

Mwezi Juni, waandaaji walisema kumekuwa na mahitaji yaliyoweka rekodi ya tiketi wakati huo zilipouzwa tiketi milioni 1.2. Kiwango hicho sasa ni maradufu.

SOMA NA HII  KUELEKEA RATIBA YA ROBO CAF....TIMU VIGOGO AFRIKA ZAIKATAA SIMBA MAPEMAAA....YANGA MHHH...