Home Habari za michezo KUELEKEA RATIBA YA ROBO CAF….TIMU VIGOGO AFRIKA ZAIKATAA SIMBA MAPEMAAA….YANGA MHHH…

KUELEKEA RATIBA YA ROBO CAF….TIMU VIGOGO AFRIKA ZAIKATAA SIMBA MAPEMAAA….YANGA MHHH…

Habari za Simba SC

Michezo ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika wikiendi iliopita na kupatikana timu 8 zilizofuzu kwa hatua iliyofuata.

Swali kubwa ni nani atacheza na nani, huku droo ya kupanga michezo ya Robo Fainali inatarajiwa kupangwa Aprili 5.

Kocha mkuu wa timu ya Esperance ya Tunisia, Nabil Maalou amesema yupo tayari kukutana na timu yoyote kati ya National Al Ahly au Js Kabylie,Siyo Simba sports club wekundu wa msimbazi.

Kocha huyo amesema kwa msisitizo kabisa tena kwa utuo kwamba National Al Ahly au Js Kabylie hao waleteni hata Kesho.

Akiongea kiufundi kocha huyo amesema kwamba,ratiba itambeba Simba sports club maana ataanzia nyumbani, kwa hiyo umbali wa kutoka Tanzania hadi Tunisia utamfanya akose muda wa maandaluzi kwa ajili ya mchezo wa marudiano nchini Tunisia.

Simba sports club kama watapata matokeo mazuri katika Mchezo wao katika uwanja wa (nyumbani) machinjioni taifa hawawezi kuhitaji maandalizi makubwa sana, kama timu iliyopoteza mchezo.

Hali hii pia iko kwa mashabiki wa Mamelod Sundowan ambapo wamesema kuwa Simba ni timu kubwa na ya kuogopwa katika hatua hii haswa mara baada ya kuifunga Horoya goli 7-0 kwa Mkapa.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Simba, upande wa Yanga hakuna timu yoyote iliyojitokeza kuiongelea kama ni timu tishio au yakawaida, japo ushindi mfululizo wa mechi za hivi karibuni unaifanya kuwa timu ya kuchungwa sana kweny upande wao wa kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  MASAA YA MANULA KUBAKI SIMBA YAHESABIKA...DEWJI ASHINDWA KUTOA JIBU LA MOJA KWA MOJA...