Home Habari za michezo MZINZE AMTOLEA ‘BASTOLA’ STRAIKA MPYA YANGA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

MZINZE AMTOLEA ‘BASTOLA’ STRAIKA MPYA YANGA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Yanga leo

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize amesema hatakata tamaa na kuendelea kujituma zaidi mazoezini na kufanya vizuri uwanjani ili kumshawishi kocha Miguel Gamondi kumuamini na kuendelea kumpa nafasi ndani ya kikosi cha timu hiyo

Kauli hiyo ni baada ya ujio wa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Joseph Guede ambaye amekuja kuchukuwa nafasi ya Hafiz Konkoni aliyetemwa usajili wa dirisha dogo.

Mzize amepandishwa kutoka kikosi cha timu ya vijana na sasa yuko kikosi cha timu kubwa akiungana na kinara wa mabao ndani ya kikosi hicho, Kennedy Musonda ambao walitegemewa kurithi nafasi ya Fiston Mayele anayetumikia klabu ya Pyramid.

Mzize amesema anatambua ushindani uliopo ndani ya timu hiyo katika safu ya ushambuliaji, anapambana na kujituma mazoezini na kufanya vizuri katika mechi kila anapopewa nafasi ili kuendelea kupata namba.

Amesema haitakuwa na kazi kubwa kwa sababu tayari kocha Gamondi ameshamuona na kazi kubwa anayoifanya ni kuendelea kujituma zaidi kufanya vizuri iwe katika mazoezi au mechi.

“Ni kweli katika nafasi ninayocheza kuna mtu ambaye amekuja kuleta ushindani ila kumbuka nyuma alikuwa Mayele lakini nilifanikiwa kucheza , suala la kupata nafasi ninaimani bado nitapata kwa sababu nitajituma na kufanya yale maelekezo ya benchi la ufundi ili kupata nafasi ya kucheza.,” amesema Mzize.

Ameongeza kuwa watapambana kufanya vizuri kwenye mechi zao kwa kuwa wapo tayari kuwapa furaha mashabiki na wao kutimiza malengo yao.

”Bado kuna nafasi ya kufanya vizuri na tunaamini kwamba ligi itakaporejea tutaendelea kuwapa furaha mashabiki, maandalizi ambayo tunayafanya yanatupa imani ya kuwa imara kwenye mechi zijazo na tunaamini itakuwa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Mzize

SOMA NA HII  GAMONDI AWAANGUKIA MASHABIKI WA YANGA