Home Uncategorized AZAM FC V SIMBA NI VITA YA KISASI LEO

AZAM FC V SIMBA NI VITA YA KISASI LEO

KIKOSI cha Simba, jana kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kumalizana na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.

Azam wataikaribisha Simba wakiwa wamefanya mabadiliko kwenye uongozi wao ikiwa ni pamoja na kuachana na Kocha Msaidizi Idd Cheche pamoja na Ofisa Habari, Jaffary Maganga.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu za kushinda bao 1-0 mchezo wa kwanza walipokuwa nyumbani uwanja wa Taifa.

Bao hilo la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere hivyo leo kazi itakuwa ni moja kwa timu ya Azam kulipa kisasi huku Simba ikihitaji kulinda rekodi.

Azam FC ipo chini ya Arstica Cioaba jana ilifanya pia mazoezi ya mwisho kumalizana na wapinzani wao Simba.

SOMA NA HII  SARE NNE ZAIBUA SABABU NYINGINE HUKO JANGWANI, UONGOZI WASEMA HILI NALO LINACHANGIA