Home Ligi Kuu JKT TANZANIA KUCHEZA MECHI TATU ZA KIRAFIKI

JKT TANZANIA KUCHEZA MECHI TATU ZA KIRAFIKI

KOCHA Mkuu wa Klabu ya JKT Tanzania Abdalah Mohamed,’Bares’ amesema kuwa kwa sasa kikosi hicho kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara na wanatarajia kuwa na mechi tatu za kirafiki kujiweka sawa.


JKT Tanzania kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 20 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.


Bares amesema kuwa wapo vizuri kwa ajili ya mzunguko wa pili na wanaamini kwamba ushindani utakuwa mkubwa ndani ya uwanja.

“Tunatajia kucheza mechi tatu za kirafiki ambazo zitaweza kutupa matokeo mazuri ndani ya uwanja na kwa kuanza ninadhani tutaanza na Mtibwa Sugar kisha nyingine mbili zitafuata.


“Wachezaji wapo vizuri na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara nina amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa.Tukimaliza mechi zetu za kirafiki nina amini tutakuwa na kitu ambacho tumekijenga,” .

Kwa sasa JKT Tanzania inaendelea na mazoezi bila ya nyota wake Adam Adam ambaye yupo na timu ya Taifa ya Tanzaniam Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki michuano ya Chan na kutolewa nchini Cameroon.

Inakutana na Mtibwa Sugar ambayo ipo nafasi ya 11 na pointi zake ni 22 kibindoni baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

SOMA NA HII  NAMUNGO YAPIGA HESABU KUFANYA VIZURI KIMATAIFA