Home Habari za michezo MKENYA AINGILIA DILI LA NKANE YANGA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

MKENYA AINGILIA DILI LA NKANE YANGA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Yanga

VIONGOZI wa Dodoma Jiji wameanza mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa kikosi hicho, Denis Nkane kwa mkopo kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.

Nkane aliyejiunga na Yanga Januari Mosi mwaka jana akitokea Biashara United baada ya kuonyesha kiwango kizuri ameshindwa kupenya kikosi cha kwanza tangu timu hiyo ilipokuwa chini ya Kocha Nasreddine Nabi na sasa, Miguel Gamondi.

Akizungumza juu ya taarifa hizo Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Francis Baraza aliyewahi kufanya kazi na nyota huyo alisema ni ngumu kuweka wazi juu ya hilo ingawa tayari alishaongea na viongozi kuhusu mapendekezo yake anayohitaji dirisha hili.

“Ni kweli kwenye mchezo wa Tabora United na Yanga uliochezwa hapa Dodoma nilikuwa naye ila kama unavyojua Nkane nami tunajuana sana, hivyo tulikuwa tunazungumza mambo mbalimbali ndio maana umeona watu wamekuwa wakihusisha hilo,” alisema.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Patrick Semindu alisema kwa sasa wako mapumzikoni hadi Januari 6, mwakani ila ripoti ya kocha kuhusu maingizo mapya inafanyiwa kazi hivyo suala la Nkane analisikia tu.

Hata hivyo, inafahamika kuwa Baraza anahitaji saini ya nyota huyo aliyemtengeneza akiwa Biashara na kuivutia Yanga kumsajili.

SOMA NA HII  KISA YANGA...'SURE BOY' AGOMEA MAZOEZI AZAM FC..KIBOKO YA SIMBA APIGA HODI YANGA....