Home Uncategorized HALI YA NIYONZIMA INAZIDI KUWA FRESH

HALI YA NIYONZIMA INAZIDI KUWA FRESH


KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupata majeraha jana, Julai 5 wakati wakikubali kugawana pointi moja na Biashara United.

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Shecky Mganzija amesema kuwa Niyonzima hakuumia sana hivyo leo anaweza kuanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzanke.

Yanga inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Julai 8.

“Niyonzima hajaumia sana hata leo anaweza kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar,” amesema.

Niyonzima amefunga jumla ya mabao mawili ndani ya Yanga ambapo amefunga bao moja kwenye ligi na bao moja kwenye Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA SIMBA AFICHUA SIRI ZA CHAMA NA SHEVA